Header Ads

Breaking News
recent

Bangladeshi nikiama cha watoto yatima

Serikali ya Bangladeshi imesajili maelfu ya watoto mayatima katika kambi zinazo wahifadhi wakimbizi wa Rohingya wakati maafisa na makundi ya kutoa misaada wakijaribu kutafuta mpango wa kukabiliana na wimbi la watoto hao wasiokuwa na wasaidizi.
Watoto wa Rohingya wakiwa wanangoja kupokea msaada katika kambi za wakimbizi Bangladeshi
Takriban Waislam 600,000 wasiokuwa na utaifa wameondoka nchini Myanmar tangu mashambulizi yafanywe na kikundi cha Arakan Rohingya Salvation Army, ambalo lilipelekea hatua za kijeshi zilizoelezewa na makundi ya haki za binadamu kama ni mauaji ya kimbali.
Wengi wa watu hao ambao wamekimbia ni watoto, na wengi wao wamepoteza wazazi wao huko Myanmar au wakati wakiwa njiani kunusuru maisha yao. Watoto katika vituo vya kuwasaidia watoto vya shirika la Umoja wa Mataifa la UNICEF wameweza kupata picha za kutisha za maovu ya jeshi la Myanmar katika kuvishambulia vijiji vya Rohingya, japokuwa Myanmar imekanusha katakata kuwa iliwalenga raia katika mashambulizi hayo.
Pritam Kumar Chowdhury, naibu mkurugenzi wa kitengo cha Ustawi wa Jamii huko katika eneo la wilaya ya Cox’s Bazar, amesema inawezekana kuna watoto zaidi ya 15,000, ingawa ni vigumu kuhakiki madai ya mtu mmoja mmoja wakati taarifa haziko za kujitosheleza.
“Hapa Bangladesh tunapomtambua mtoto yatima, maafisa wetu wanatembelea makazi yao ili kuthibitisha hilo. Lakini hapa haiwezekani kwenda Myanmar kuthibitisha madai hayo. Kwa hivyo chochote wanachosema tunachukua kama ni sehemu ya taarifa,” ameiambia VOA, akiongeza kuwa serikali pia inazungumza na majirani na watu ambao pengine walikuwa wamesafiri nao wakati wakikimbia kutoka Myanmar.
“Lakini hakuna ushahidi, bali tunategemea zaidi taarifa za mdomo. Tunaendelea na mkakati wetu wa kukamilisha utaratibu rasmi wa kupata taarifa kamili. Hatuwezi kudai kuwa tuko sahihi kwa asilimia 100 lakini siyo kwamba orodha hii yote haiko sahihi.

Jean-Jacques Simon, msemaji wa UNICEF, amesema katika barua pepe kuwa kati ya watoto 14,740 waliosajiliwa na serikali ya Bangladeshi kama “mayatima” nusu ya kesi hizo zimefanyiwa marejeo na tayari zimeingizwa katika kumbukumbu za Wizara ya Ustawi wa Jamii.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.