Header Ads

Breaking News
recent

pata chimbika kesi ya lulu mahakamani

Kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili msanii wa fani ya uigizaji filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu Lulu inaendelea leo Jumatano Oktoba 25,2017 katika Mahakama Kuu.

Askari wa Kituo cha Polisi Oysterbay Sajenti Nyagea amefika mahakamani kutoa ushahidi. Shahidi huyo ndiye aliyerekodi maelezo ya Josephine Mushumbusi.

Jaji Sam Rumanyika anayesikiliza kesi hiyo aliiahirisha jana Jumanne Oktoba 24,2017 na kuamuru polisi aliyerekodi maelezo ya Mushumbusi kufika mahakamani.

Kabla ya Jaji Rumanyika kutoa amri hiyo, Wakili Peter Kibatala anayemwakilisha Lulu katika kesi hiyo aliieleza Mahakama Kuu kuwa Mushumbusi hapatikani kwa kuwa yuko nchini Canada, hivyo aliiomba Mahakama iyapokee maelezo yake kama sehemu ya ushahidi.

Wakili wa Serikali, Faraja George alisema hapingi kuwasilishwa maelezo hayo mahakamani, bali anapinga kuwasilishwa na wakili Kibatala kwa kuwa yeye si aliyeyarekodi.

Lulu ambaye yupo nje kwa dhamana anakabiliwa na kesi ya kumuua bila ya kukusudia msanii wa filamu, Steven Kanumba.

Anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 7, 2012, nyumbani kwa marehemu Kanumba, Sinza Vatican jijini Dar es Salaam.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.